Jumatano , 14th Jan , 2015

Staa wa filamu hapa Bongo, Vicent Kigosi 'Ray' ameirushia lawama Serikali kupitia chombo chake cha bodi ya filamu kuzuia baadhi ya filamu ambazo hugusa mambo muhimu katika jamii hususan yale ya kisiasa, kwa hofu ya kulinda maslahi yake binafsi.

Muigizaji wa bongo movies Vicent Kigosi aka Ray

Ray amesema haya akitolea mfano wa kuzuiwa kwa filamu yake inayokwenda kwa jina Sister Mary ambayo kwa mujibu wake inagusia ukweli unaoendelea katika mambo ya dini, na kusema kuwa mpaka sasa hapa nchini bado hakujaweza kuwa na wigo mpana wa kuzungumza ukweli wa mambo.