Alhamisi , 13th Nov , 2014

Aliyekuwa rapa mkali wa muziki wa Hip Hop Bongo, Geez Mabovu amezikwa leo huko Iringa katika makaburi ya Makanyagio katika tukio lililovuta mamia ya waombolezaji wakiwepo wasanii na mashabiki wa muziki.

msanii wa muziki wa bongofleva nchini marehemu Geez Mabovu

Kuhusiana na maziko hayo Man Simple, Rafiki wa karibu pamoja na msanii aliyefanya kazi kwa karibu na marehemu kwa muda, akiongea nasi kwa njia ya simu kutoka Iringa.

Marehemu Geez Mabovu, ameacha majonzi makubwa kwa wapenzi wa Hip Hop ambao wameshiriki kutoka ndani na nje ya mkoa huu kutoa ya moyoni kwa namna walivyomfahamu rapa huyu kwa njia ya sanaa zake.

eNewz tunaitakia roho ya marehemu Geez Mabovu mapumziko mahala pema peponi, Amin.