Jumamosi , 10th Mei , 2014

Mwigizaji kutoka Nigeria, Ramsey Nouah ameendelea kutikisa anga za kimataifa katika fani yake ya uigizaji, ambapo safari hii staa huyu ametokea katika show ya uhalisia ya muendelezo ya "Love & Hip Hop Atlanta, ambayo hutengenezwa nchini Marekani.

Kuonekana kwa staa huyu katika show hii, ni moja kati ya hatua kubwa kabisa katika fani yake, na mpango huu umekuja kama suprise kwa mashabiki wake ambao hawakuwa wanafahamu chochote mpaka hatua ya mwisho ambapo staa huyu anatokea katika shoo hii.

Ramsey ambaye amekuwa kinara wa filamu huko Nigeria kwa zaidi ya miaka 10 sasa, ameendelea kujiimarisha zaidi katika fani hiyo kimataifa, ambapo kwa sasa kazi zake nyingi anazifanya nnje ya mipaka ya Nijeria, hususan Marekani.