Jumapili , 10th Oct , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za kuwapongeza wasanii wa BongoFlava Diamond Platnumz, Alikiba, Nandy, Rosa Ree, Marioo na Zuchu kwa kuchaguliwa kuwania tuzo za AFRIMMA 2021.

Picha ya Rais Samia Suluhu Hassan kushoto, kulia ni msanii Diamond

Rais Samia amewapongeza wasanii hao 6 katika Uzinduzi wa Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa kupambana na Uviko19 kwa kusema tuwape moyo, tuwaunge mkono na tuwapigie kura kwa wingi ili kuweza kushinda tuzo hizo.

Pia amempongeza bondia Hassan Mwakinyo na timu ya wanawake Twiga Stars kwa kuchukua ubingwa wa COSAFA siku ya jana.