Ijumaa , 7th Aug , 2015

Rais wa Tanzania, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza nia yake ya kujitolea kusaidia kuinua sekta ya sanaa katika kipindi chake, kuwa ni baada ya kujionea hali halisi ya kundi hilo katika jamii kuwa haipo sawa ukilinganisha na nchi nyingine.

Rais wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete

Rais Kikwete amesema hayo katika hafla ya kuagana na wasanii iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, akiahidi serikali kufanya kitu kubadilisha maisha ya wasanii ambao hujituma na kuitangaza sanaa yao nje ya nchi.

Baada ya hotuba hiyo, baadhi ya wasanii wakiwemo Cassim mganga na Fid Q ambao wametoa shukrani kwa kauli na hatua hiyo ya Mheshimiwa Kikwete.