Jumatano , 29th Oct , 2014

Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini na pia aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Mheshimiwa, Ismail Aden Rage leo hii ameweza kuchat Live na wapenzi wa ukurasa wa facebook wa EATV, kupitia kipengele chatu maarufu cha Kikaangoni Live.

Mhe. Ismail Aden Rage akichat Kikaangoni Live leo

Mheshimiwa Rage ambaye kwa upande wa Burudani ameweka wazi mapenzi yake kwa Bendi ya Msondongoma, amejibu maswali mbalimbali, na baadaye kukutana na eNewz na kuzungumzia mambo ya burudani kidogo na kutaja wasanii wa muziki wa kizazi kipya anaowakubali ambapo amemtaja Shilole, Diamond na Ali Kiba katika orodha hii.

Mheshimiwa Rage amesema kuwa, yeye binafsi ni mpenzi mkubwa wa muziki na Anamiliki Bendi kutoka huko Tabora (Tabora Jazz) ambayo mara zote wabunge wanapokuwa Vikaoni Dodoma, huwepo kwaajili ya kuwatumbuiza.