Alhamisi , 11th Jun , 2015

Jitihada za rapa wa Kenya, Rabbit aka Kaka Sungura kuupeleka mbele zaidi muziki wake zimeendelea kuonekana, hasa baada ya kufanikiwa kukutana na staa wa muziki 2 Face kutoka Nigeria na kuweka mipango sawa.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Rabbit akiwa na 2 Face Idibia

Rabbit kwa njia ya mtandao ameweka picha akiwa na msanii huyo ambaye yupo Kenya kwa sasa, na uongozi wake kutoa taarifa kuwa kuna mpango mzito unapikika kutokana na mkutano huo.

Rabbit kwa sasa anajipanga kuachia kazi kadhaa ambazo amezifanya akishirikiana na wasanii wengine, ikiwepo ninaweza aliyoshirikishwa na Avril, pia Slow Down ambayo ameifanya na Roberto kati ya rekodi nyingine.