Quick Rocka
Enews ilimuuliza Rack sababu za kuita wimbo wake mpya mwendo kasi na alikuwa na haya ya kusema
'MIMI NI MTU AMBAYE NAPENDA VITU VIENDE FASTA FASTA SIPENDI MIYEYUSHO NDO MAANA NIKAAMUA KUIMBA MWENDOKASI ILI WATU WAJUE KAMA TUNAFANYA KAZI TUFANYE NA SIO MIZINGUO ZINGUO' alimalizia hivyo Quick.
Hata hivyo Qick ameeleza jinsi anavyoweza kufanya kazi na msanii chipkizi Chin Bzz na ilishawahi kusikika Chin Bzz akimlalamikia Nall kuwa alikuwa hamlipi licha ya kutoa idea nyingi za nyimbo katika studio za Nall na alikuwa na haya ya kusema
"Chin yupo katika studio yangu na anasaidia sana katika kutoa idea za beat pale anapotengeneza produza Lufa".
Hata hivyo Rocka amesema wanamlipa Bzz vizuri na watu wategemee vitu vizuri kutoka kwa dogo huyo kwani inawezekana kwa asilimia kubwa kwamba mafanikio yake yalipangwa yapatikane katika studio za Switch Raka na watu wategemee nyimbo nzuri zaidi kwani hata ngoma yake ya mwendo kasi Bzz alikuwa moja kati ya watu waliotoa idea mbalimbali.
