Jumanne , 10th Aug , 2021

Switcher Baba Quick Rocka amesema yeye sio msanii wa kufuata mziki wa 'trending' kama Amapiano unaofanya vizuri Bongo kwa sasa na nia yake ni kufanya mziki ambao utaishi milele.

Picha ya msanii Quick Rocka

Akizungumzia hilo mbele ya camera za EATV & EA Radio Digital Quick Rocka anasema muziki wa trending ni wa mpito tu sio unaoishi.

"Ni sawa kwa kinachoiendelea lakini ukiangalia mpangilio wangu sijawahi kufanya 'trending music' naamini ni muziki fulani wa mpito, mimi huwa napenda kufanya kitu kinachoishi ndio maana nyimbo zangu za miaka iliyopita zinasikilizika, uta-enjoy na zina vibe".

Kwa sasa Quick Rocka ameachia EP yake mpya ya 'Love Life' ambayo ina ngoma nne baada ya ukimya wa miezi 16 bila kuachia kazi yoyote.