Jumatano , 30th Sep , 2015

Nyota mkongwe wa Bongofleva, Q Chief amesema kuwa kutokana na kuelewa hamu kubwa ya watanzania sasa kutaka kumjua Rais wao, ataleta mapinduzi kipindi kifupi baada ya hilo kwa kuachia track yake iitwayo chawa.

Nyota mkongwe wa Bongofleva, Q Chief

Kwa mujibu wa kauli ya Q Chief ambaye amekwishaonyesha dhahiri kupania kuweka kileleni heshima na nafasi yake katika muziki kwa mashambulizi ya kazi mpya na zenye ubora kila baada ya kipindi kifupi, kupitia mahojiano yake na eNewz, bila kufafanua kwa undani kama anahusisha kazi yake hiyo na siasa zinazoendelea sasa, Chawa itakuwa ni mapinduzi mengine makubwa baada ya watanzania kumjua Rais wao ni Nani.