
Q Chillah ndani ya Planet Bongo ya EA Radio
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Q Chief amesema yeye kama mmoja ya wasanii ambao wametoka mbali na kituo hicho cha utangazaji cha East Africa Television na East Africa Radio, wanajivunia kuona leo imefikia hatua hiyo, hivyo wasanii wengine wanatakiwa kuthamini hilo.
"Nawaambia wenzangu kuwa wajichukulie kama watu wenye thamani na wamethaminiwa, tumetoka mbali na EATV, kulikuwa na circumstance, sacrafice nyingi ila zote ili to do the best, wathamanini hili kama wameamua kuingia, ni muhimu sana katika taifa hili na kwenye industry, na kama unavyojua tuzo zinatoa changamoto, kwa sababu hutegemei tuzo moja peke yake, tunatarajia zitakuwa nyingi hivyo ni fursa kwao", alisema Q Chief.
Wasanii ambao wamefanikiwa kupenya kwenye kinyang'anyiro cha EATV AWARDS wanaanza kuwekwa hadhrani leo hii na baada ya siku chache zoezi la upigaji kura litaanza.