Jumatano , 1st Apr , 2015

Msanii wa nchini Kenya Prezzo ambaye amekuwa kimya kwa muda kuhusiana na upande wake katika mahusiano ya kimapenzi ameamua kutoa picha rasmi akiwa amemkumbatia msichana na kuwashangaza mashabiki wake kwa kutwitti maneno ya mapenzi.

Msanii wa muziki wa nchini Kenya Prezzo akiwa na msichana mrembo

Imeelezwa kuwa wawili hao wamekuwa karibu na kuonesha hisia zao mbele ya umma kwa kujiachia kimahaba ambapo staa huyo hakutaka kuweka wazi jina la mrembo huyo ambaye ameanza kuteka vichwa vya habari nchini humo.

eNewz inakupatia maneno hayo ya mahaba yaliyosomeka katika akaunti ya twitter ya Prezzo kama ifuatavyo: Even when the stars would break, she would rub me on my back and say babie it’ll be ok#Empress #MyHommieLoverAndFriend #QueenWithTheCrown.