Ijumaa , 29th Mei , 2015

Baada ya msanii wa muziki G-Snake kutoka nchini Uganda kushambuliwa na kuumizwa vibaya na promota wa muziki anayefahamika kwa jina Frank Jay almaarufu kama DJ Frank, polisi nchini humo wanaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo.

msanii wa muziki wa nchini Uganda G-Snake

Kwa mujibu wa Ronald kalibbala ambaye ni mume na pia meneja wa msanii huyo, tukio la shambulizi la mkewe limetokea baada ya kukataa kufanya onesho katika tukio ambalo alialikwa na kulipwa kwa makubaliano ya kuhudhuria peke yake na si kutumbuiza.

Kwa sasa G-Snake anaendelea kuuguza majeraha wakati Frank akiendelea kujificha kusipojulikana, upande wa mashtaka ukipambana kuhakikisha kuwa anapatikana na sheria inachukua mkondo wake.