
Picha ya P Mawenge
P Mawenge anasema kitendo hicho kilimfanya kuachwa na mpenzi wake huyo waliodumu kwenye mahusiano kwa kipindi cha miaka minne japo alijitahidi kujitetea lakini ikashindikana.
"Kuna mwanamke alinitumia picha WhatsApp sasa mpenzi wangu akaona picha za ajabu ajabu zinaingia iliniletea matatizo sana, ni mtu ambaye tulikuwa tumezoeana mpaka mnazinguana halafu ile miyayusho inakuja kudondokea kwenye wakati usio rasmi au sahihi"
Aidha msanii huyo ameongeza kusema "Niliachika kwa sababu ya drama unajua ulimwengu wa sasa hivi una sababu nyingi sana za watu kugombana kwenye mahusiano na utandawazi ndio umeleta matatizo tofauti na zamani".