Jumatatu , 9th Jun , 2014

Rapa mkali wa michano kutoka nchini Nigeria, Phyno ameweka wazi kuwa anamkubali na kumpenda sana msanii wa maigizo Genevieve Nnaji, na ana ndoto za kutoka naye kimapenzi siku moja.

Phyno akiwa na Genevieve Nnaji

Phyno amesema kuwa, ana matumaini kuwa anaweza kuwa na mahusiano na mwanadada huyu mashuhuri kutokana na imani kuwa, hakuna kinachoshindikana chini ya jua.

Rapa huyu ambaye kumekuwa na tetesi juu ya kuwa na mahusiano na msanii mwenzake Chidimna, amewahi pia kuweka wazi suala la yeye kumtaka Genevieve kimapenzi hata kupitia baadhi ya mashairi katika nyimbo zake.