
Petitman Wakuache akimvalisha pete ya uchumba mpenzi wake
Petitman Wakuache amepost video akimvalisha pete mpenzi wake akiwa leba huku akisindikiza caption inayosema 'I love you Official Dodo mama yake Petit Junior'.
Petitman amefanya hivyo baada ya mpenzi wake huyo kujifungua mtoto wa kiume ambaye wamempa jina la Petit Junior siku ya jana baada ya kushea habari hizo kwenye page yake ya instagram.
Huyo anakuwa mtoto wa pili kwa Petitman baada ya Baby Taraj wakuache aliyempata akiwa na Esma Platnumz.