Jumamosi , 3rd Mei , 2014

Siku kadhaa baada ya taarifa juu ya ugomvi ndani ya kundi la P Square, ambao ulizua hofu ya kuvunjika kwake likiwa katika kilele cha mafanikio, Moja ya wasanii kutoka kundi hili, Peter Okoye amekiri kuwa ni kweli kulikuwa na ugomvi kati yao.

Peter, Paul na familia

Peter amesema kuwa, ugomvi ulioibuka kati yao ni kama ambavyo inaweza kutokea kwa watu wengine wowote ambao ni ndugu, na sasa umekwisha, ingawa hakutaja sababu rasmi za kutokea kwa ugomvi huu uliofanikiwa kuviteka vichwa mbalimbali vya habari vilivyo.

Ugomvi huu pia umehusishwa na mpango wa wasanii hawa kujaribu kutafuta kiki ya kutangaza ujio wa albam yao mpya, katika wakati huu ambapo wamekuwa katika mishe za kutengeneza video ya ngoma ya Testimony nchini Afrika Kusini.