Jumatatu , 1st Apr , 2024

Mwanamuziki wa Dansi kutoka Congo DR anayeishi Tanzania Nyoshi El Sadaat anasema pesa alizotumia kwenye kupaka mkorogo unaweza kujenga nyumba nyingi.

Picha ya Nyoshi El Saadat

“Toka nimeanza kutumia mkorogo mpaka leo kwa kukadiria naweza kununua nyumba nyingi”.

“Nimeingia Tanzania 1992 mpaka leo natumia natumia Mkorogo ni pesa ngapi? Usifikiri natumia mkorogo wa Elfu 50 au 40, mkorogo wangu kuanzia laki 3 au Laki 2”.

Pia ameongeza kutamba kuwa hata miwani anayovaa ni gharama kubwa sana kuanzia Tsh Milioni 1 kwa sababu ni Original sio zinazopitishwa mitaani na barabarani.

Nyoshi El Sadaat alikuwa member wa bendi ya FM Academia na sasa ni rais Bogoss Music.