Jumatano , 28th Jan , 2015

Mwigizaji mahiri wa nchini Uganda, Patrick Idringi ametupilia mbali shavu alilopata la kufanya kazi ya filamu na timu kutoka Hollywood Marekani kutokana na madai ya kuvunjiwa heshima yake mara kwa mara na Mtayarishaji wa filamu hiyo.

Mchekeshaji maarufu wa nchini Uganda Patrick Idringi

Idringi amesema kuwa kabla ya kuchukua uamuzi huo, amevumilia mara kadhaa kushushiwa hadhi yake akiwa na matumaini ya kupata uzoefu mpya kufanya kazi na muongozaji filamu kutoka Hollywood, kazi ambayo ameshindwa kuendelea nayo.

Star huyu mwenye kipaji kikubwa cha kufanya vichekesho amesema kuwa, anaamini kuwa atapata nafasi nyingine kubwa na nzuri kwa upande wa kazi hiyo huku akiweka wazi kuwa kwa sasa ameamua kujikita katika kuendeleza shughuli zake za vichekesho peke yake.