Jumatatu , 13th Nov , 2023

Baada ya Harmonize kushinda tuzo 3 za African Entertainment Awards USA (AEAUSA) amesema anajianda kufanya paredi ya mapokezi ya tuzo hizo kuanzia Airport mpaka nyumbani kwake Konde Village.

Picha ya Harmonize na meneja wake Jembe ni Jembe

"Tangu muziki wetu au niseme sanaa yetu ianze sikumbuki lini mara ya mwisho msanii toka Tanzania kulipatia hili Taifa la Mama Samia tuzo 3 za kimataifa ndani ya usiku mmoja".

"Moja au Mbili nakumbuka ila 3 sina kumbukumbu kwahiyo paredi litaanzia Airport mpaka Konde Village halafu tunakesha mpaka asubuhi. Soon nawarudia na tarehe pamoja na saa ninayotua. Kondegang's ni muda wenu wa kutamba".

Tuzo hizo 3 alizoshinda Harmonize ni Artist of the year, Best music video (Single Again) na King of East Africa and Afro-BongoFlavour.