Jumapili , 6th Jul , 2014

Msanii mkongwe anayekubalika zaidi nchini Zimbabwe na nje ya Zimbabwe Oliver Mtukudzi amepatiwa shahada ya heshima ya udaktari kutokana na moyo wake wa upendo anaouonesha kwa binadamu.

Mwanamuziki Oliver Mtukudzi wa Zimbabwe

Shahada hiyo ya udaktari imetolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Ubinadamu ambapo mbali na Mtukudzi pia watu kadhaa walitunukiwa udaktari wa heshima kwa michango yao iliyosaidia maisha ya wananchi wa Zimbabwe.

Akizungumzia kuhusu tuzo hiyo Mtukudzi amesema amefurahi mno kutunukiwa udaktari na kuongeza kuwa anajivunia mno kuona kazi anayoifanya kusaidia maisha ya watu wengi ikitambuliwa na watu wengine, jambo ambalo alikuwa hatarajii.