
Octopizzo
Video hii inatarajiwa kuwa kivutio cha aina yake pindi itakapotoka na pia itakuwa ni production ya kwanza ya aina hii kwa msanii kutoka Afrika Mashariki Kufanya, ikiwa ni mchakato wa msanii huyu kutaka kuleta tofauti katika sanaa.
Video hii ni ujio mwingine mkubwa kabisa wa Octopizzo ingawa mpaka sasa bado kiasi cha pesa ambacho msanii huyu amewekeza katika kufanya kazi hii hakijafahamika, na wala jina la kazi yenyewe.