Jumanne , 18th Nov , 2014

Msanii wa muziki Nuh Mziwanda ameweka wazi kuwa, rekodi yake ya Msondongoma ambayo ndiyo imemtoa ni kati ya rekodi mbili alizokuwa anafikiria kuziachia.

msani wa muziki wa kizazi kipya nchini Nuh Mzwanda

Na kwa utafiti aliofanya kwa wadau, rekodi hii haikuwa chaguo lao kuwa kazi ya kwanza kwa msanii huyu kutoka nayo.

Nuh Mziwanda amesema kuwa, aliamua kuachia Msondongoma kutokana na msukumo aliokuwa nao binafasi, akiacha ushauri alioupata, na kwa kuzingatia hili, mafanikio aliyopata ni makubwa kuliko alivyokuwa anatarajia.