
Msomi na Msanii wa muziki Noah PV
Hii inakuwa ni moja ya kazi bora yenye ujumbe unaowataka watanzania kuwa sehemu ya maamuzi ya mustakabali wa nchi yao kutokana na kutambua umuhimu wa kupiga kura kuelekea katika uchaguzi mkuu mwezi ujao.
Noah PV, ameeleza kuwa rekodi ya ushiriki hafifu wa watanzania katika uchaguzi katika kipindi cha nyuma ndio moja ya sababu kubwa zilizomsukuma kufanya kazi unayoitazama sasa kama anavyoeleza mwenyewe hapa.
