Wasanii wa lebo Konde Gang kutoka kushoto ni Country Boy, Ibraah Tz, Harmonize, Killy na Cheed
Akifunguka suala hilo kwenye kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio inayorushwa kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa 7:00 mchana hadi 10:00 jioni Country Boy ameeleza kuwa
‘‘Mara ya mwisho kuachia kazi yangu ilikuwa ni Album ya Yule boy, baada ya kuachia hiyo nilikuwa nimejipanga kwa ajili ya hii EP yangu halafu ujue mimi nilikuwepo pale Konde Gang kama miezi 11 iliyopita kabla ya kutambulishwa ’’
Pia Country Boy amewapa sifa kundi la OMG kwa kusema huu ndiyo wakati wao wakutamba kwani HipHop ya Tanzania inatakiwa kufika hadi nchi za nje, ‘‘Hasira ambayo wanayo OMG ni kubwa sana kwenye huu muziki na HipHop ya Tanzania inatakiwa itoke nje kwa hiyo huu ndiyo muda wao, mfano kama Young Lunya alipata ushawishi kutoka kwa Chidi Benz"