Witness
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Witness amesema kwa siku nyingi baadhi ya wasanii wanakosa kutambulika mchango wao kutokana na uchache wa tuzo, hivyo amewaomba Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kutoa vibali kwa watu wengine, ili kuweza kuwa na tuzo nyingi zaidi zitakazoleta hamasa zaidi kwenye kazi za sanaa.
“Kuna wengine wanakosa kuwekwa kwenye tuzo zingine kwa sababu ya nafasi hakuna, lakini hii kitu mimi nawapongeza sana East Africa kwa kweli, kwa sababu hii kitu itaongeza ushindani, na natamani pia hata media zingine zinaweza zikafanya hivi, hata watu binafsi pia wanaweza wakawa na awards zao, lingine naomba tu BASATA wawapatie vibali kama njugu, i'm so happy highly kiukweli”, alisema Witness.
Witness aliendelea kusema kwamba kwa mara ya kwanza alivyosikia kuhusu EATV AWARDS, alijawa na furaha isiyoelezeka huku akiruka ruka.
“kiukweli kabisa naweza nikasema kati ya watu ambao wamefurahia East Africa Awards, mimi nimefurahia sana, kwa mara ya kwanza nimeipata hizi taarifa I was like waoo!! yani I jumped from the coach, unajua ni kwa sababu nimeshaenda nchi mbali mbali, nimekuta watu wana tuzo hadi za kipindi cha radio, sisi Tanzania nzima tuna tuzo moja!! hii haiwezi ikakuza vipaji na vipaji siku hizi viko vingi”, alisema Witness