Jumatatu , 7th Apr , 2014

Mtayarishaji muziki na rapa kutoka Black Curtains Records, Mswaki Mabeats ambaye ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina 'Makeke', amesema kuwa, kwa sasa ameamua kufanya ujio wake rasmi akiwa kama yeye mwenyewe.

Mswaki

Producer na rapa huyu ameamua kufanya hivi kuonyesha tofauti ya kazi ambazo ametanguliza hapo awali ambazo alikuwa akiimba kwa sauti kama ya marehemu Ngwair.

Mswaki amesema kuwa, Makeke ambayo inawakilisha neno la Kiingereza 'Swagg', amefanya na Mwasiti kwa ajili ya kuwapatia watu nafasi ya kumsikia akirap kama yeye, ambapo amesema kuwa hii haimaanishi kuwa project ya "Keeping Ngwair Alive" inayohusisha kazi zake alizofanya kama Ngwair ikiwepo ngoma ya Ghetto, imefika kikomo.