Jumatatu , 5th Mei , 2014

Mkali wa michano ambaye anafanya poa hapa Tanzania, Nikki Mbishi a.k.a Nikki Zohan, ambaye katikati ya mwaka huu anatarajia kuachia albam yake mpya 'Ufunuo', amesema, hatua yake ya kuachia albam hii ni kipimo cha ukubwa wa uwezo wake katika rap.

Nikki Mbishi

Nikki Mbishi amesema haya kutokana na imani inayoendelea sasa kwa wasanii na wadau wa muziki kuwa biashara ya albam za muziki hususan wa Bongoflava na Hip Hop hailipi, na kuhusiana na hili, hapa anaelezea juu ya alivyojipanga na albam hii.

Msanii Nikki Mbishi amesema kuwa, wasani wengi hapa nchini wanaogopa kutoa albam kwasababu ya kutokuamini uzuri wa kazi zao, na pia kutokana na kutokupenda kazi zao tofauti na yeye ambaye anaajiamini na kuamini kuwa kazi yake ni nzuri na ni biashara tosha.