Alhamisi , 16th Nov , 2023

Mwanamuziki wa Kenya Brown Mauzo anasema siku akifariki hataki watu kumzungumzia au kumpost mitandaoni ili kuonesha hisia zao kama wanampenda kwa sababu hataona huo upendo ikiwa hayupo.

Picha ya Brown Mauzo

Brown Mauzo anasema kama kweli watu wanampenda wanaweza kumuonyesha huo upendo akiwa bado yupo hai kwa kumpigia simu au kumtumia ujumbe sio wasubiri akifariki.

"Kwa familia yangu ya mitandao ya kijamii, Nikifa msinipost kwenye mitandao ya kijamii jinsi ulivyonipenda. Kama una upendo wa dhati utanipigia/tuma ujumbe mfupi au nitumie DM sasa na uniambie unavyohisi kunihusu. Nionyeshe sasa na nipende sasa". ujumbe wa Brown Mauzo