Alhamisi , 29th Jan , 2026

Moja ya story inayotrend Marekani kwa sasa ni rapa Nicki Minaj kuonyesha hadharani kumuunga mkono Rais wa Marekani Donald Trump akisema ni Rais wake kipenzi na bora wa muda wote.

Picha ya Rais Trump na msanii Nicki Minaj

Baada ya Nicki kutoa kauli hiyo kwenye video wakiwa pamoja Rais Donald Trump akajibu kwa kumsifia akisema msanii huyo ni malkia wa Rap/HipHop.

Pia Nicki Minaj alipewa zawadi ya kazi ya dhahabu kutoka kwa Rais Trump kwenye mkutano wa kudumu wa Akaunti ya Trump.

Kadi hiyo ya Dhahabu ni ya Visa kulingana na uwezo wa mtu binafsi wa kutoa manufaa makubwa kwa Taifa la Marekani.