Jumatano , 10th Feb , 2016

Msanii wa Bongofleva Ney Wa Mitego ameingia tena kwenye midomo ya watu wengi.

Ney Wa Mitgo

Baada ya kuachia wimbo wake mpya wenye vijembe vingi kwenda kwa wasanii wenzake akiligusa hadi Baraza la Sanaa BASATA, akijitetea kuwa vijembe vyote hivyo ni katika jitihada zake kueleza hali halisi inayoendelea katika tasnia ya burudani.

Ney huwataja watu maarufu kwenye nyimbo zake kitu ambacho watu wengi huchukulia ni kama kiki tu, wengi wakidhani kuwa anakosea, ila hapa Ney anatetea msimamo na maamuzi yake.