Nedy Music
Baada ya Mubenga kuitosa PKP na kuanzisha lebo yake mpya ya Bangers, Msanii wake wa zamani Nedy Music aeleza hisia zake juu ya Mubenga.
Nedy Music kwa sasa amebaki chini ya usimamizi wa Ommy Dimpoz tu katika lebo hiyo ya PKP. Nedy amesema hana tatizo lolote na aliye kuwa Meneja wa lebo hiyo Mubenga japo kwa sasa hafanyi naye kazi tena.
Akinzungumza na eNewZ Nedy anasema 'Mimi sifahamu kama kuna tatizo kati yetu, kwa hiyo nazungumza naya kama kawaida. Sisi tupo kikazi zaidi kama wasemavyo mtani ni “mfeto mfeto”.
Mwisho Nedy alimaliza kwa kushukuru mashabiki wake wanaendelea kumsapoti pia waendelee kusubiri vingi vizuri kutoka PKP maana wamejipanga kikazi zaidi.








