Nay ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo 'PB' inayorushwa na East Africa Radio baada ya msanii mwenzake Godzilla kuwa wa kwanza kutuikubali wimbo wa mikono juu na kudai ni mbaya na vitu vingine vingi.
"Mimi nimechukulia kama ni mtazamo wake tu japo siwaimbii wasanii wenzangu, najua watu wangu wanahitaji kitu gani na ndio maana tukienda katika 'show' huwa nakuwa mshindi wa kwanza kwa sababu nawajua mashabiki zangu. Siwezi kununa wala 'kum-maindi' Godzilla kwa kauli yake", amesema Nay
Kwa upande mwingine, Nay wa Mitego amesema mwaka huu 2018 amekuja na mwendo wa kupiga kazi ili kuweza kuufikisha mbali muziki wake.

