Jumamosi , 29th Nov , 2014

Kutoka Uganda, rapa Navio amesema kuwa yupo katika mchakato wa kubadilisha upepo wa muziki wa Rap na Hip Hop Afrika Mashariki, na hii itakuwa ni kupitia albam yake mpya ambayo itasimama kwa jina la Power.

Navio

Kazi hiyo itashirikisha wasanii kadhaa kutoka hapa Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashatiki.

Navio amesema kuwa, kupitia project hii kwa mara ya kwanza kabisa anajipanga kwaajili ya kuizindua katika nchi Tano za Afrika Mashariki kwa mara moja, ujio ambao utakuwa ni wa kihistoria katika soko la muziki, Something About You, video unayoicheki kwa background sasa ikiwa ni moja kati ya kazi za awali kutoka Albam hiyo.