
Upande wa kulia ni Baba Levo, kushoto ni Peter Msechu
Akizungungumza na EATV & EA Radio Digital, Baba Levo amesema huwa anajisikia raha pale anapomshambulia Peter Msechu na lengo lake ni kumtaka akonde na kumpa mawazo.
"Najisikia raha ninapomshambulia Peter Msechu, lengo la kumshambulia huwa nataka akonde na nimpe mawazo ili awe na mwili flani hivi kama Vanessa Mdee, nataka hata akitembea awe sawa na Vanessa, ila siwezi nikamtania hadi kumvunjia mipaka yake kwa mfano kufika hadi kwa wazazi" amesema Baba Levo .