
Mwana FA ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kueleza kuwa video hiyo itaanza kuonyeshwa kwenye televisheni zinazoonekana Afrika nzima na kisha ndio yeye ataweza kuiachia.
“Ni kweli video imekamilika almost, kwa sababu walikuwa wanaleta second cuts jana usiku, kuna marekebisho mawili matatu na kila kitu kitakuwa tayari, kwa hiyo nilikuwa nasubiri jamaa wanipe kalenda yao kwamba inaanza kuonyeshwa kwenye televisheni zinazoonekana afrika nzima lini alafu ndo tutakuwa tunaweza kurelease hiyo ngoma”, alisema Mwana FA.
Mwana FA ameendelea kusema kwamba kwa sasa hivi anahakikisha anaendena na soko la kimataifa, na kwamba kazi zake za sasa zimedhihirisha kwamba anakua kisanaa.
“Ninachokifanya over the years ni kuhakikisha kwamba nakuwa, mi nashindana na mi mwenye, unashindana na kasi ya dunia lakini unashindana na viungo vyako mwenyewe, ninachotaka kusema ni kwamba project yangu mpya imeendelea kudhihirisha hiyo trend yangu kwamba najaribu kukua”, alisema Mwana FA.