Jumamosi , 12th Nov , 2022

Rais wa Manzese Music Baby (MMB) Madee ameshea ujumbe wake kwa msanii Kontawa ambaye anafanya vizuri na goma ya Champion kwa kueleza ukimtoa Maarifa msanii wa kuzingatiwa mwaka 2023 ni Kontawa.

Picha ya Madee kushoto, kulia ni Kontawa

Madee ameandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Instagram ukieleza kuwa "Oya 2023 azingatiwe huyu nadhani ndio mnoma kwa sasa ukimtoa Maarifa Big Thinker. Narudia tena Kontawa azingatiwe".

Kupitia lebo yake ya MMB Madee tayari ameshatoa vichwa kadhaa kwenye game kama Dogo Janja, Maarifa na Gazza.