Ijumaa , 7th Mar , 2014

Mrembo Nancy Sumari kupitia taasisi yake ya Neghesti Sumari, imeandaa jukwaa la majadiliano ya masuala mbalimbali katika yahusuyo mapambano dhidi ya gonjwa la UKIMWI, ujasiriamali na uongozi katika kusherekea s

Hii ni moja ya jitihada kubwa ambazo anafanya mrembo huyu katika nafasi yake kama kioo cha jamii, katika kujaribu kuyaangazia masuala mbalimbali ya kumnyanyua mwanamke katika jamii, yakiwepo pia masuala ya usawa na afya ya uzazi.

Harakati hizi ni katika kuleta chachu zaidi kuelekea siku ya kesho, Machi 8 ambayo ndiyo itakuwa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.