Jumatano , 9th Apr , 2014

Msanii wa muziki, Nameless kutoka nchini Kenya, ametolea ufafanuzi jina la albam yake mpya Before I Retire (B4IR), kuwa haimaanishi kuwa yupo katika mpango wa kustaafu muziki kama wengi ambavyo wanatafsiri.

Nameless amesema kuwa, jina la albam hii limetokana na ukimya wake wa muda mrefu ambao umepelekea wengi kufikiri kuwa amekwishastaafu na kuachana na muziki, na hapo ndipo alipoamua kurejea na kazi yenye jina kama hili kuonyesha kuwa anaendelea na ataendelea kufanya muziki zaidi kabla ya kustaafu.

Nameless amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, kuna vitu vingi zaidi ambavyo anatarajia kufanya katika muziki kabla ya kufikia hatua ya kustaafu.