Ijumaa , 13th Nov , 2015

Msanii wa Hip Hop ambaye amekuwa gumzo baada ya kuachia video yake ya Don't Bother na kuwa gumzo Joh Makini, amesema analazimika kugharamia kwa kiasi kikubwa video zake anazofanya, ili azidi kujitangaza kwenye soko la muziki kimataifa.

Joh Makini ameyasema hayo ndani ya Planet Bongo ya East Africa Radio alipoenda kutambulisha wimbo wake huo wa Don't Bother, na kusema kwamba kwa sasa ameshafika hatua ya kimataifa, hivyo ni lazima afanye video zenye hadhi ya kimataifa.

"Kwa level ambazo naenda za kimataifa natakiwa kulipa pesa kubwa kwa video, gharama ya don't bother ni dola 9000, including models na production, lakini ukiongeza na shopping zetu mavazi na vingine jumla dola 15000", alisema Joh Makini.

Joh Makini amesema video hiyo imemfanya kuvunja rekodi ya video zote alizofanya, na kuzidi kumtengenezea njia nzuri.

"Nimevunja tena rekodi yangu, ngoma ya Don't Bother imeshacross ni moja ya ngoma inayotrend kwenye tasnia ya muziki ya South Africa", alisema Joh Makini.

Pamoja na hayo Joh Makini ameizungumzia kolabo yake na Davido ambayo inatarajiwa kutoka siku za hivi karibuni, na kusema kuwa kabla hawajafanya nyimbo hiyo, Davido ndiye aliyekuwa akimtafuta Joh Makini bila mafanikio, na hatimaye kuamua kumtafuta yeye.

"Davido alikuwa ananiulizia sana, mi nasikia tu Davido anakuulizia, nahisi alikuwa hajui atanipataje nikaamua kumtafuta, na nakumbuka siku hiyo niliingia kwenye instgram yangu nikakuta alinitumia DM, yoooh lets work...", alisema Joh Makini.