
Lulu Diva kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EATV alisema anajutia kuingia kwenye fani hiyo kwani imekuwa ikiwashushia heshima kutokana na baadhi ya video queen kufanya mambo ya ajabu katika jamii jambo ambalo linawafanya watu kuona wote wapo sawa.
"Ni bora hata ingekuwa kutongozwa lakini mimi najutia kuwa video queen kwa sababu kuna baadhi ya video queen wamekuwa matendo mabaya, wanapiga piga picha za uchi hovyo, na namna wanavyoishi katika jamii wanapelekea watu wote kuona kuwa Video queen ni watu wenye tabia mbovu" alisema Lulu Diva
Mbali na hilo Lulu Diva alisema kuwa kazi hiyo pia haina maslahi yoyote yale kwani pesa wanazopewa na wasanii ni pesa kidogo sana ambayo haiwezi kuwafanya kupiga hatua yoyote ile
"Wasanii wanatakiwa kujua umuhimu wa video queen maana ni muhimu lakini pesa wanazokuwa wanawapa video queen ni ndogo sana na hailingani na kazi ambayo wanakuwa wamefanya kwenye video zao" alisisitiza Lulu Diva