Alhamisi , 13th Dec , 2018

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wanaowakilisha kundi la Navykenzo, Aina na Nahreel, wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni baada ya miaka kadhaa ya uhusiano wao.

Taarifa za ndoa hiyo zimewekwa wazi na Nahreel kwenye ukurasa wake wa instagram wakati akisheherekea siku yake ya kuzaliwa, akiwa pamoja Aika mjini Cairo nchini Misri, kwa kuandika ujumbe uliosomeka wazi kuwa harusi yao itafungwa hivi karibuni.

 

More Life More Love, Lov You aikanavykenzo Soon Wedding 

A post shared by Nahreel (@nahreel) on

Aina na Nahreel wapo kwenye mahusiano zaidi ya miaka 7 sasa, ambapo katika uhusiano wao wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume anayejulikana kwa jina la Gold, ambaye ametimiza mwaka mmoja hivi karibuni.