Alhamisi , 9th Feb , 2017

Rapa anayechipukia kwenye muziki wa Hip hop 'Basaga' ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Badilisha pozi' amefunguka na kusema kuwa toka anaanza kufanya muziki watu wamekuwa wakimfananisha kimuziki na Nay wa Mitego.

Pamoja na kufananishwa huko, rapa huyo anasema sasa amekuja kuchukua nafasi ya Nay wa Mitego kama hatajipanga vizuri. 

Basaga anasema ni kweli Nay wa Mitego anafanya vizuri kwenye muziki lakini anaamini wimbo wake unaokuja sasa 'Natafuta baunsa' utakuja kumuondoa kabisa Nay wa Mitego kwentye masikio ya watu na kufanya watu wamsikilize yeye. 

Msanii Becka Title akiwa na Basaga 

 

Tazama video hii Basaga akifunguka mengi zaidi, anasema anahitaji Nay wa Mitego na Kalapina kuwa mabaunsa wake yaani watu wa kumlinda.

Tazama video ya ngoma yake hapa