Msanii wa muziki wa Bongofleva Chege Chigunda
Chege amesema kuwa anapoenda kupiga picha za video za track zake ama kuingia studio za nje hufanya hivyo kutokana na kutafuta kitu cha ziada na wala si kwa ajili ya kufuata magorofa mazuri, bali ni kuongeza mashabiki nje ya Tanzania.
Akizungumzia suala la umuhimu wa makundi ya muziki Chege amesema kuwa umoja ni nguvu ila hata hivyo wasanii katika makundi wanapaswa kuheshimiana pamoja na kila mmoja kuwa na uwezo wa kukubalika hata akisimama mwenyewe.