Hussein Machozi ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Afica Rdaio, na kueleza kuwa kwa kuwa amekuwa busy na majukumu mengine, ameamua kuacha muziki na kujikita zaidi kwenye shughuli hizo.
“Kubwa ambalo nataka niwaambie Tanzania leo hii ni kwamba very soon nitaachia ngoma yangu mpya ambayo ni ya mwisho kabisa kwa Hussein Machozi, namaanisha naacha muziki naacha bongo fleva nakuwa mtu wa kawaida ambaye nitaishi maisha yangu ya kawaida, sababu ya kuwa hivyo ni kwamba kuna kitu ambacho kikubwa nakifanya kwenye maisha yangu, ambacho kitanibadilishia maisha yangu kiurahisi, na pia nafanya hivyo kwa sababu ya heshima ya watanzania”, alisema Hussein Machozi.
Husssein Machozi ameendelea kwa kusema kuwa anajisikia vibaya kutokana na uamuzi wake lakini hana jinsi, kwani kwa sasa huwezi kufanya kitu ambacho hakikuiingizii pesa.
“Nasikia vibaya sana na inaniumia lakini no way out I have to go, kuna kitu kikubwa nakifanya kwenye maisha yangu, kwa sababu ukiangalia kwa haraka haraka huwezi endelea kufanya kitu ambacho hakikuingizii”, alisema Hussein Machozi.
Pamoja na hayo Hussein Machozi amegusia suala la wasanii wengi kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, na kusema kuwa wengi hufanya hivyo kutokana na mawazo na maisha magumu yanayowakabili.
“Hizi mambo za kuingia kwenye madawa ya kulevya, watu hawaingii kwa sababu ya arosto au wanapenda, wanaingia kwenye madawa ya kulevya kwa sababu ya stress, watu wanajiuliza kwa nini wanamuziki wanaingia kwenye masuala kama haya, wapo wengi lakini wanamuziki imekuwa ni janga kubwa, ni stress tu hamna kitu kingine”, alisema Hussein Machozi

