Jumanne , 22nd Apr , 2014

Msanii mkongwe wa muziki hapa Tanzania, Mzee Ally Zahir Zorro amesema kuwa kwa sasa yupo katika mpango wa kuirudisha bendi yake ya Mass Media kwa kasi katika muziki, ambapo sasa anawajengea wanamuziki wake nyumba ambayo itawasaidia kukaa pamoja.

Mzee Zahir Zorro

Mzee Zorro amesema kuwa ,mpango huu umekuja baada ya kukaa kwa muda mrefu na kujionea changamoto mbalimbali za kuendesha bendi, kubwa ikiwa kukaa mbali kwa wanamuziki na sasa ameamua kuachana na kazi nyingine zote na kuwekeza katika mpango huu mkubwa.

Msikilize Mzee Zorro hapa akielezea mpango huu mzima;