Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mzee Yusuph ataka nyimbo zake zifutwe

Ijumaa , 26th Mei , 2017

Aliyekuwa mfalme wa muziki wa miondoko ya pwani 'taarab', Mzee Yusuph amewataka watu wote waliokuwa na nyimbo zake kwenye simu wafanye hima kuzifuta kwa madai wakiendelea kuzisikiliza watampatisha dhambi katika hilo.

Mzee Yusuph

Mzee Yusuph amefunguka hayo ikiwa ni masaa machache yamebakia kwa waumini wa dini ya kiislamu kuanza ibada yao ya kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

"Mimi nikikubali watu wacheze nyimbo zangu ina maana nimeruhusu dhambi tena ni bora nirudi kuimba muziki tena, hivyo watu wote waliokuwa na nyimbo zangu kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza ili kuepuka dhambi....Nimetenda sana makosa tena hadharani na kila mtu anajua lakini kwa sasa ninawaomba tu mniombee dua ili niendelee kuwa salama japo hali yangu kiuchumi haiko sawa imebadilika nazidi kupambana ili kipatikane kitu" alisema Mzee Yusuph

Aidha, Mzee Yusuph amesema kwa sasa hajihusishi na masuala ya muziki wa kidunia tena bali ataendelea kuitangaza dini yake pamoja na kuimba nyimbo za kaswida.

Pamoja na hayo, Mzee Yusuph amewasihi waislamu kumrudia Mungu wao kwa kufanya mambo mema katika kipindi hiki cha mfungo pamoja na kuwataka akina baba kuacha manyanyaso kwa wake zao majumbani.

HABARI ZAIDI

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji