Jumatano , 29th Jul , 2015

Aliyekuwa nguli katika tasnia ya maigizo Kenya, Marehemu Mzee Ojwang' anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Langata huko Kenya, baada ya kufariki dunia takriban siku 17 zilizopita sababu kubwa ikiwa ni kushambuliwa na homa ya mapafu.

Aliyekuwa nguli katika tasnia ya maigizo Kenya, Marehemu Mzee Ojwang'

Nafasi ya wasanii na wadau kukutana kuenzi maisha ya Mzee huyo ilitolewa jana Nyayo Stadium, ambapo siku ya leo waombolezaji wote watashiriki katika maziko yake Jijini Nairobi.

Msiba wa mzee huyo ulioonekana kuondoka katika kumbukumbu za watu, sababu ikiwa ni ujio wa Rais Obama Kenya, ikiwa sasa limebaki jukumu moja tu la kumsindikiza kwa heshima katika mapumziko yake ya milele.