Jumanne , 26th Mei , 2015

Staa wa filamu Niva ameweka wazi kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa kufanya muziki akiwa tayari anajulikana kama mwigizaji, amejipanga vizuri na ana malengo makubwa ya kupiga hatua kwa kuziunganisha fani hizo mbili.

Niva

Kupitia mahojiano tuliyofanya naye, Niva amesema kuwa katika siku za mbeleni kupitia sanaa yake ana mpango wa kufanya mashabiki wake kujipatia nakala ya filamu kila wakiingia katika onesho lake la muziki.

Vile vile staa huyo akaweka wazi uwekezaji mkubwa alioufanya katika muziki, kwa kufanya kolabo na staa mkubwa wa Uganda ambaye hakuwa tayari kumtaja jina lake, akitarajia kwenda kufanya video ya kazi hiyo Afrika Kusini hivi karibuni.