Jumatatu , 19th Aug , 2019

Msanii wa HipHop na Mfanyabiashara hapa nchini Tanzania Mwana Fa, amenyoosha maelezo juu ya watu wengi kulitaja  jina lake kama linaweza kuingia kwenye siasa.

Mwana FA

Msanii huyo amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital ambapo amesema,

"Sijui nini kinawafanya watu waamini kama naweza kuingia kwenye siasa, lakini huwezi jua zote ni kadari tu sijajua nilichopangiwa kufanya kesho. Naamini chochote nitakachoamua kufanya kitakuwa ni manufaa ambayo sio yangu tu ni kwa jamii nzima".

Aidha Mwana Fa ameendelea kusema  kuwa hawezi kusema kama anaweza au hawezi kuingia kwenye siasa kwa sababu  suala hilo lipo katikati.

Licha ya kazi ya usanii na ufanyaji biashara Mwana Fa ni mjumbe wa bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), pia ni mmoja wa watu maarufu ambao wana ushawishi mkubwa hapa Tanzania.

Aidha Mwana Fa ambaye jina lake la utani ni "James Bond" amesema bado anauwezo wa kucheza ngumi ulingoni na anaweza akapanda ulingoni kupambana kwa raundi zote 12.